Monday, April 3, 2023

Tanzania yasaini mkataba kupambana na malaria

 


Dar es Salaam. Wakati Serikali ikiendelea kupambana na ugonjwa wa malaria, Wizara ya Afya imesaini hati ya makubaliano ya kushirikiana na Kampuni ya SCJohnson iliyopo Marekani kwa lengo la kupambana na ugonjwa huo.

Makubaliano hayo yalisainiwa jana, Aprili 2, 2023 yakihudhuriwa na Makamu Mtendaji wa Rais wa Shirika hilo, Mark Martin, Balozi  wa Umoja wa Viongozi wa Nchi za Afrika dhidi ya Malaria (ALMA), Anthony Okara pamoja na Mwenyekiti Mteule wa Baraza la kutokomeza ugonjwa huo nchini, Mhandisi Leodgar Tenga.

 Kampuni hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wamesaini hati ya kuwasaidia wananchi wa Tanzania katika kupambana na ugonjwa wa malaria.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search